Katika jamii pana inafahamika kuwa mwanamke akiingia kwenye ndoa huwa
anatulia na kujipanga kwa ajili ya familia na maendeleo kwa jumla.

Hali ni tofauti kabisa kwa staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman.
Aunt ana utofauti mkubwa na wanandoa wengine kwani maisha anayoishi
tangu aingie kwenye ndoa na Sunday Demonte, hayana tofauti na yale
aliyokuwa akiishi kabla hajaingia kwenye ndoa miaka miwili iliyopita.
Aunt amekuwa akijiachia sehemu mbalimbali za starehe bila kujali kama ni mke wa mtu na amekuwa akikumbwa na skendo lukuki.
Hali hiyo imekuwa ikiwashangaza wengi na kujiuliza kweli ni mke wa mtu?
Katika makala haya utaona matukio mbalimbali ambayo Aunt amewahi
kuyafanya tangu aingie kwenye ndoa ambayo si kitu cha kawaida kwa
mwanandoa.
KUKAA NUSU UTUPU JUKWAANI Siku chache baada ya
kufunga ndoa, mwaka 2012, Aunt alikwenda kwenye shoo ya Fiesta mjini
Dodoma akiwa ameambatana na Wema Isaac Sepetu na kufanya kituko cha
mwaka.
Akiwa kwenye shoo hiyo, Aunt alipanda jukwaani akiwa nusu utupu
ambapo alipigwa picha ambazo zilizua gumzo kwenye vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii. Ishu ilikuwa iweje mke wa mtu afanye hivyo bila
aibu?
Skendo hiyo ilimfanya Aunt na Wema kutengwa na Shirikisho la Filamu
(TAFF) lakini baadaye waliomba msamaha na kupewa onyo wasirudie kuvaa
hivyo na endapo wangerudia wangeondolewa kabisa kwenye listi ya wasanii
wa Tanzania.
KUPIGWA CHUPA Mwaka jana ndani ya Klabu ya
Bilicanas iliyopo Posta, Dar, Aunt alipasuliwa na chupa mkononi baada ya
kumkosakosa usoni na aliyetekeleza unyama huo ni mwanadada
aliyejulikana kwa jina la Yvonne Maximilian ambaye kabla ya Aunt kuingia
kwenye ndoa walikuwa wakimgombea mwanaume aitwaye Geofrey.
Japokuwa Aunt alishaingia kwenye ndoa bado skendo hiyo ya kutembea na
huyo mwanaume ilikuwa ikimsumbua Yvonne akihisi kwamba mwanadada huyo
anaendelea na Geofrey, jambo ambalo Aunt alisema siyo kweli na
waliachana muda mrefu kabla hata hajaingia kwenye ndoa.
SKENDO YA KUJIUZA Hivi karibuni Aunt alikumbwa
na skendo ya kujiuza baada ya kwenda jijini Arusha akiwa ameambatana na
Wema na Kajala Masanja ambako walienda kwenye shoo ya kumtambulisha
msanii wa Bongo Fleva, Mirrow kutoka kampuni ya Wema ya Endless Fame
Films.
Ilidaiwa kwamba nyuma ya ziara hiyo kulikuwa na mabilionea waliowaita
jijini humo ambao pia walifurika kwenye shoo hiyo iliyofanyika katika
Ukumbi wa Tripple A.
KUPIGANA Mapema mwaka huu, Aunt alijikuta
akizichapa na mwanamke aitwaye Sarah Mwakapala ambaye miaka kadhaa
iliyopita waliwahi kugombea naye penzi la mwanaume aliyejulikana kwa
jina la Mwilu Mwilola ‘Silva’.
Chanzo cha wawili hao kuzichapa hadi kuvuana mawigi hakikueleweka
lakini Aunt alishtuka baada ya kuvamiwa na mwanadada huyo wakiwa katika
sherehe kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo Victoria, Dar.
Aunt anapaswa kubadilika na kuonesha sifa za mke wa mtu.