Aunt ana utofauti mkubwa na wanandoa wengine kwani maisha anayoishi tangu aingie kwenye ndoa na Sunday Demonte, hayana tofauti na yale aliyokuwa akiishi kabla hajaingia kwenye ndoa miaka miwili iliyopita.
Aunt amekuwa akijiachia sehemu mbalimbali za starehe bila kujali kama ni mke wa mtu na amekuwa akikumbwa na skendo lukuki.
Hali hiyo imekuwa ikiwashangaza wengi na kujiuliza kweli ni mke wa mtu?
Katika makala haya utaona matukio mbalimbali ambayo Aunt amewahi kuyafanya tangu aingie kwenye ndoa ambayo si kitu cha kawaida kwa mwanandoa.
KUKAA NUSU UTUPU JUKWAANI
Siku chache baada ya kufunga ndoa, mwaka 2012, Aunt alikwenda kwenye shoo ya Fiesta mjini Dodoma akiwa ameambatana na Wema Isaac Sepetu na kufanya kituko cha mwaka.
Akiwa kwenye shoo hiyo, Aunt alipanda jukwaani akiwa nusu utupu ambapo alipigwa picha ambazo zilizua gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ishu ilikuwa iweje mke wa mtu afanye hivyo bila aibu?
Skendo hiyo ilimfanya Aunt na Wema kutengwa na Shirikisho la Filamu (TAFF) lakini baadaye waliomba msamaha na kupewa onyo wasirudie kuvaa hivyo na endapo wangerudia wangeondolewa kabisa kwenye listi ya wasanii wa Tanzania.
KUPIGWA CHUPA
Mwaka jana ndani ya Klabu ya Bilicanas iliyopo Posta, Dar, Aunt alipasuliwa na chupa mkononi baada ya kumkosakosa usoni na aliyetekeleza unyama huo ni mwanadada aliyejulikana kwa jina la Yvonne Maximilian ambaye kabla ya Aunt kuingia kwenye ndoa walikuwa wakimgombea mwanaume aitwaye Geofrey.
Japokuwa Aunt alishaingia kwenye ndoa bado skendo hiyo ya kutembea na huyo mwanaume ilikuwa ikimsumbua Yvonne akihisi kwamba mwanadada huyo anaendelea na Geofrey, jambo ambalo Aunt alisema siyo kweli na waliachana muda mrefu kabla hata hajaingia kwenye ndoa.
SKENDO YA KUJIUZA
Hivi karibuni Aunt alikumbwa na skendo ya kujiuza baada ya kwenda jijini Arusha akiwa ameambatana na Wema na Kajala Masanja ambako walienda kwenye shoo ya kumtambulisha msanii wa Bongo Fleva, Mirrow kutoka kampuni ya Wema ya Endless Fame Films.
Ilidaiwa kwamba nyuma ya ziara hiyo kulikuwa na mabilionea waliowaita jijini humo ambao pia walifurika kwenye shoo hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Tripple A.
KUPIGANA
Mapema mwaka huu, Aunt alijikuta akizichapa na mwanamke aitwaye Sarah Mwakapala ambaye miaka kadhaa iliyopita waliwahi kugombea naye penzi la mwanaume aliyejulikana kwa jina la Mwilu Mwilola ‘Silva’.
Chanzo cha wawili hao kuzichapa hadi kuvuana mawigi hakikueleweka lakini Aunt alishtuka baada ya kuvamiwa na mwanadada huyo wakiwa katika sherehe kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo Victoria, Dar.
Aunt anapaswa kubadilika na kuonesha sifa za mke wa mtu.
No comments:
Post a Comment