Staa wa Bongo Fleva, Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’.
BAADA ya kupotea kwa muda, huku wengi wakishindwa kutambua anaishi
wapi na nani, hatimaye picha za staa wa Bongo Fleva, Mbwana Mohamed ‘Mb
Dog’ na familia yake zimenaswa!Kutokana na desturi ya staa huyo kukaa ‘mbali’ na kamera husan katika masuala yahusuyo familia, paparazi wetu alimuotea nyumbani kwake Kawe, jijini Dar na kumtandika picha kadhaa kabla ya kumfanyia mahojiano.
Licha ya kuonekana kutopenda kuanika sana mambo yake ya kifamilia, Mb Dog aliyewahi kutamba na wimbo la Latifa, alifunguka kwa kifupi kuwa, aliyekuwa naye ni mkewe na amebahatika kuzaa naye watoto wawili.
“Hapa ndiyo maskani, siku zote naishi na mke wangu wa ndoa pamoja na hawa watoto wawili,” alisema Mb Dog.
Hata hivyo, alipobanwa zaidi na paparazi kufafanua kuhusu maisha yake, jina la mkewe na la watoto alipatwa na kigugumizi ghafla, hakuwa tayari kufunguka.
Kuhusiana na changamoto anazokutana nazo, Mb Dog alisema muda mwingi anakuwa mbali na familia pindi anapokuwa amekwenda kupiga shoo.
“Kama unavyoniona, kuna wakati napata shoo nje ya nchi, inabidi tu kuacha familia na huko nachukuwa muda wa wiki mbili hadi tatu na wakati mwingine mwezi mzima kurudi.
“Si unajua mtu ukishakuwa staa lazima ufuatiliwe na watoto wa kike sasa ndipo balaa linapoanzia,” alisema Mb Dog.
No comments:
Post a Comment