Mkurugenzi wa Mtendaji wa
Kampuni ya Aj It Development Bw Jackson Audiface akizungumzia kuhusu
Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali yatakayofanyika Mkoani
Dododma Mwezi Aprili mwaka huu. Maonyesho hayo ya kazi za Vijana
wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya Dodoma. Lengo la
Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa Tanzania.
Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana Wajasiriamali Ili
kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli zao za
Ujasiriamalia.Bidhaa
Mbalimbali za Kilimo Zinazozalishwa na Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao
watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.Bw
Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika
Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana
wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao
walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya
Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana
wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Akikagua Moja ya Shuguli za Kikundi
cha Vijana kijulikanacho Kama Mae Ambao watashiriki Katika Maonyesho
hayo.
Kampuni
ya AJ IT DEVELOPMENT inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za
vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth
Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 - 5
April, 2014 Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu Mkurugenzi wa
Kampuni ya AAj It Development Bw Jackson Audiface, Maonyesho hayo ya
aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye lengo la Kuzitangaza Kazi za
Vijana Wajasiriamali.
“Maonyesho haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
“Maonyesho haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
Aliongeza kuwa washiriki
watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu Mbalimbali na Namna Ya
Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa Wingi zaidi.Namna ya
Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali
za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha Bidhaa zao ziendane na
soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya Wateja.
Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.
Washiriki wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali Wanazofanya Vijana. Pili kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao.
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda.
No comments:
Post a Comment