Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini,
Jokate Mwegelo amefunguka kwa kusema kuwa ameamua kufungua biashara ya
ndala za brand yake ya ‘Kidoti’ kutokana na mapenzi yake ya uvaaji wa
ndala kataki maisha yake ya kawaida .
“Mimi napenda kuvaa ndala, napenda kuvaa wakati nakwenda
kushoot,siwezi kuvaa high hills wakati nashoot, wakati unapakwa make up
unaonaee, unatengenezwa nywele, you cannot wear hills lazima uwe umevaa
kitu comfortable,”.“Kwahiyo nikaona kwamba ndala ni kitu kizuri,napenda kuvaa ndala,ni kitu easy,kuvaa rahisi halafu ni kitu ambacho watu wanakihitaji why not have ndala ambazo zina mvuto wa kipekee? Kama nilivyohaidi watu kwamba Jokate kupitia brand ya Kidoti itaanzisha bidhaa mbalimbali kukidhi mahitaji ya watu na jamii mzima.
Nashukuru kuna support kwa Kidoti yenyewe kama brand. Kwahiyo tutaendelea kutoa vitu mbalimbali vya kufurahisha. Unajua kutoa surprise ni njia moja wapo ya kufurahisha, hawakutegemea kupata kitu kuzuri lakini wamekipata. Kwahiyo ni mambo ya Kidoti hayo ni bidhaa nzuri waipokee na tutaendelea kutoa bidhaa mbalimbali.” aliongeza.
Pia Kidoti amesema kuwa bidhaa ya ndala ya Kidoti itapatikana Tanzania nzima.
“Tutasambaza Dar es salaam nzima na mikoani,kwahiyo ni kitu ambacho kipo katika mipangilio ya kusambambaza sehemu mbalimbali ili upatikanaji uwe rahisi na tunafanya jitihada za kutangaza sehemu ambazo zitakuwa zinapatikana.”
No comments:
Post a Comment