MUIMBAJI
mahiri na Kiongozi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Luiza
Nyoni Mbutu amesema kwa jinsi mambo yanavyokwenda katika dunia ya sasa,
anafikiria kuachana na bendi hiyo na kuwa mama wa nyumbani tu.
Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, Luiza alisema imefika mahali anawaza kuwa mama wa nyumbani kwa sababu amegundua katika dunia mtu akiwa kiongozi hasa kuongoza vijana kama wa kwenye bendi hiyo changamoto zinakuwa nyingi katika maamuzi.
“Mimi ni kiongozi wa Twanga Pepeta, lakini nafikiria siku moja kuachana na bendi na kukaa nyumbani kulea wanangu.
“Kuongoza vijana kuna changamoto nyingi sana. Umri wangu kwa sasa si wa kukutana na mambo ya vijana japokuwa mume wangu (Fariala Mbutu) anazijua changamoto hizo na kuzikubli,” alisema Luiza.
Luiza alianza kuimbia bendi hiyo mwaka 1999 na tangu wakati huo hajawahi kuhama na amekuwa nembo ya bendi nje na ndani ya nchi.

No comments:
Post a Comment