Kikosi cha TSN Boys.
TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka
dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika
Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.
Mechi hiyo itakayochezwa saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu
zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali
zitakazoanza Jumatatu ijayo.
TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na
wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali.
Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.
Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi
nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande
wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times
dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya
Tumaini Media.
TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa
kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu" ameahidi
kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000.
"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.
Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo.
"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.
Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo.
Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo Leo
walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh
Mohammed.
Bao la Jambo Leo lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto
ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya
sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora
mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).
Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari
Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global
Publishers kwa
mabao 27-8.
No comments:
Post a Comment