Stori: MAYASA MARIWATA
MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema yupo kwenye mikakati ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Siwema baada ya kumtundika mimba.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema anajivunia kukaribia kuitwa baba na kizuri ni kwamba msichana aliyempa mimba alikuwa na ndoto za kumuita mke wake hivyo ndoa itafungwa kabla ya mtoto kuzaliwa.
“Kikubwa naomba Mungu mipango yangu iende kama nilivyopanga kwa sababu nataka kabla mtoto hajazaliwa tuwe ni wanandoa tunaotambulika kwa Mungu kwa kufunga pingu za maisha,” alisema Nay.
Akizungumzia kubebeshwa mimba na msanii huyo, Siwema aliliambia Ijumaa: “Najisikia furaha sana kumbebea mimba Nay, tumetoka mbali naamini ndoto yetu ya kuoana itatimia siku si nyingi.”
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment