KIMENUKA! RB namba KT/RB/1178/2014-KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO
inamsaka staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’ kwa tuhuma ya kutishia kumuua mdogo wake aliyetajwa kwa jina la
Amani Shija, Ijumaa Wikienda limeinyaka.
Staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano nyumbani kwake, Manzese jijini Dar.
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na Shija ulianza zaidi ya miezi
mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni walikuwa maeneo ya Kijitonyama,
Dar, wakipata chakula cha usiku na marafiki zao wengine ndipo ghafla
dogo akajichanganya na kujikuta akiropoka neno lililomuudhi Nay,
akapaniki.
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki, Nay alianza kumfokea Shija na
kutishia kumuua, ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga chozi.

Akaendelea
kueleza kuwa hata baada ya siku hiyo, Nay aliendelea kumtumia SMS za
kutishia kumuua ambazo bado anazo kama ushahidi Baada ya kudaka mchongo
huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia ni msanii wa Bongo
Fleva na kumuuliza juu ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na kaka
yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay amekuwa akiendelea kumtishia kumuua jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.

Alisema
ili kujilinda ndipo alipoamua kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha
Polisi Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha kufunguliwa jalada la kesi
namba KT/RB/1178/2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila mafanikio lakini kwa mujibu wa mtu
wake wa karibu, baada ya kujua msala huo ametorokea nchini China.
No comments:
Post a Comment