Kama kawa ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazi wetu, Musa Mateja
‘Toz’, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100, zamani Mzee wa Mapikipiki’, Dustan
Shekidele ‘Mzee wa Mji Kasoro Bahari’, Shakoor Jongo ‘Zungu Fedha,’
Haruni Sanchawa ‘Cheusi’ na Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos walijiachia
viwanja mbalimbali kusaka matukio na kumrushia live kidigitali, Mkuu wao
aliyekuwa Makao Makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga Mwenge jijini Dar
es Salaam.
Mkuu akiwa ofisini kama kawaida anaangalia saa yake ya mkononi na
kubaini kuwa ni zaidi ya saa 3 usiku hivyo anamtwangia kijana wake, Musa
Mateja ‘Toz’ aliyempanga kwenye onesho la Machozi Bendi, Ukumbi wa
Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dar.
Saa 3:12 usiku
SHAMSA FORD ANASWA AKIKATIKA
Makao Makuu: Mateja najua upo kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge hapo
Namanga kama nilivyokupanga unafuatilia kwa makini shoo ya Lady Jaydee,
sijui unaweza kuniambia sasa vituko vinavyoendelea hapo?
Mateja: Yeah, hujakosea kiongozi wangu maana ni kweli nipo hapo na sasa Lady Jaydee yupo jukwaani anaporomosha burudani.
Makao Makuu: Oke, vipi suala zima la watu wapo wa kutosha maana hali ya hewa ya mvua wengi wamesimama kwenda viwanja.
Mateja:Kiukweli watu wapo wa kutosha maana shoo inafanyikia ndani na
kwamba kuna usalama wa kutosha hata kama mvua itanyesha kubwa kiasi
gani?
Makao Makuu: Kuna mastaa gani hapo?
Mateja:Karibu yangu namuona Shamsa Ford tena kapendeza ileile na
anazungusha nyonga kwelikweli nahisi ameshapiga maji ya zamzam maana
kila mtu anamkodolea macho utafikri yuko kwenye mashindano. Yaani bahati
yake yupo na bwanaa’ke angekuwa peke yake wajanja wenye hela zao
wangemnasa.
Makao Makuu: Sawa Mateja piga kazi ngoja nimcheki, Dustan Shekidele ‘Mzee wa Mji Kasoro Bahari’.
Saa 4:56 usiku
MACHANGUDOA WAFILISI MSINGI WA MUUZA KUKU
Shekidele: Naam Mkuu wangu nakupata sawia.
Makao Makuu: Haya niambie uko wapi na nini kinaendelea?
Shekidele: Mkuu nilikuwa ndani ya Ukumbi wa Makuti hapa Msamvu kwenye
onesho la Kundi la Jahazi Modern Taarab lakini nikatonywa umbeya.
Makao Makuu: Umbeya upi huo?
Shekidele: Hapa nilipo ukivuka
barabara kuna eneo maarufu la machangu karibu na gesti ya Itigi kuna
mfanyabishara wa kuku kutoka Singida aliingia gesti na changu lakini
katika mazingira ya kutatanisha changu alipoondoka jamaa akajikuta laki
nane zake zilizokuwa kwenye waleti yake hazipo.
Makao Makuu: Duh, sasa kafanyaje?
Shekidele: Mkuu hapa ni kilio tu, jamaa analia kama mtoto anasema
kuku wenyewe aliwachukua kwa mali kauli huko kwao Singida hivyo hajui
atasemaje.
Makao Makuu: Kiranga kimemponza huyo acha aingizwe mjini, ngoja niwasiliane na Shakoor Jongo ‘Zungu Fedha’.
Saa 6:18 usiku
MLEGEZO WAMPORONYOKA BLAZAMENI MBELE YA WAKWE
Shakoor: Naam Mkuu wangu habari za Ijumaa Kuu?
Makao Makuu: Salama kijana, hebu niambie uko pande zipi?
Shakoor: Mkuu niko ndani ya Ukumbi wa Escape One hapa Mikocheni yaani hapa ni kama mamtoni kuna nyomi la vijana linakula ujana.
Makao Makuu: Dah, huo ukumbi naupendaga sana yaani upo ufukweni kabisa, vipi kuna vituko gani hapo?
Shakoor: Mkuu kuna familia imekuja kula ujana hapa sasa kuna
brazameni alivaa suruali mlegezo kwa bahati mbaya wakati akijishaua
kutembea kwa miondoko ya kisharobaro bega moja juu lingine chini huku
akikanyaga hatua kama mguu mmoja mbovu mlegezo wake umemporonyoka tena
mbele ya shemeji zake na wazazi wa mchumbaa’ke.
Makao Makuu: Ayaa duh, aibu sana lakini akome kuvaa milegezo. Ukipata
mpenyo mpige picha, ngoja nimsake Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos.
Saa 7:15 usiku
Bukos: Naam Mkuu nakupata sawia, kama ulivyonipanga niko hapa Ukumbi wa Cheetoz.
Makao Makuu: Nini kinaendelea hapo?
Bukos: Mkuu Bendi ya Mashujaa Musica ‘Watoto wa Mamaa Sakina’ wanafanya makamuzi.
Makao Makuu: Umeona kituko gani hapo?
Bukos: Nimemshuhudia dada mmoja ananyonyana juisi na wanaume karibu
watano kwa nyakati tofauti, hivi tunavyoongea amebanwa kwenye kona yenye
mwanga hafifu na mwanamuziki wa hii bendi, Raja Raza nahisi naye
anataka kumpa juisi.
Makao Makuu: Mmh huyo labda anasambaza virusi vinavyosababisha homa
ya ini, achana naye ngoja nimsake, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’.
Saa 8:29 usiku
MZUNGU AMMWAGIA DOLA BANANA
Makao Makuu: Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ nafikiri uko pande za Club
East 24 kwenye onesho la B Band, hebu nijuze umeshanasa vituko gani
hapo?
Mnally: Mkuu kuna kali moja ya mwaka imetokea hapa.
Makao Makuu: Enhee, endelea Mnally nakusikia…
Mnally: Kuna Mzungu mmoja mrefu sana anammwagia Madola Banana kisa,
kamkuna na kibao kinachoitwa London Beats kilichopigwa na Kenn Thomas,
huyu mtasha anasema kinamkumbusha familia yake iliyopo kwao (Uingereza).
Makao Makuu: Sawa Mnally piga kazi, ngoja nimsake Haruni Sanchawa ambaye yuko doria maeneo ya Ukonga.
Saa 8: 56 usiku
VIJANA WA KOVA WAIMARISHA ULINZI KILA KONA
Sanchawa: Naam Mkuu wangu nakupata, kama ulivyonipanga nimepita maeneo
ya Gereza la Ukonga, FFU na sasa niko kwenye bwalo la maofisa wa
magereza, kwa kweli huko hali ni shwari, vijana wa Kamanda Kova
wameimarisha ulinzi kama kawaida yao hasa kwa nyakati kama hizi za
sikukuu.
Makao Makuu: Vipi kuna vituko ulivyoviona?
Sanchawa: Mkuu kweli mapenzi yana nguvu, hivi tunavyoongea nipo
maeneo ya bwalo la maofisa wa magereza, namuona afisa mmoja wa FFU
amepigwa makofi kama matatu na kisichana, hivi tunavyoongea huyu afisa
amekalishwa kwenye kiti na haka kasichana eti hakamruhusu kwenda popote
kisa wivu. Huyo mheshimiwa nasikia kaoza kabisa kwa haka kabinti ndiyo
maana kanamtesa.
Makao Makuu: Aah huo uzoba sasa kupenda gani huko? FFU wanavyoogopeka
halafu yeye afisa mzima anakuwa zoba. Najua hapo kupiga picha
haiwezekani we chukua data tu ukimaliza wapigie wenzako uwaambie
mkapumzike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment