KATIKA hali ya kushangaza, inaelezwa kuwa saa chache kabla ya kifo chake, staa wa filamu za Kibongo, marehemu Adam Kuambiana alipita katika baa mbalimbali za jijini Dar es Salaam kuaga mashabiki wake.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Kuambiana zinasema kuwa, Ijumaa (siku moja kabla ya kifo chake) alionekana baa mbalimbali akizungumza na mashabiki wake, jambo lililoashiria kuwa ni kama alikuwa akiwaaga.
“Alikwenda Shikamoo Pesa (Sinza Kwaremmy), Green Park (Mwenge), New Sinza (Kwa Remmy) Igo (Sinza Mori) ambapo alikaa hadi usiku wa manane. Alionekana mchangamfu sana na alizungumza na watu wengi sana siku hiyo. Ni kama alijua angekufa ndiyo maana akaamua kuagana na mashabiki wake,” alisema.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment