PEACE! Baada ya wasanii wawili waliokuwa wanaunda
Kundi la Scorpion Girls, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ na Isabela Mpanda
kuwa kwenye bifu kwa miezi kadhaa, hatimaye wamepatana.
Wasanii
wawili waliokuwa wanaunda Kundi la Scorpion Girls, Miriamu Jolwa ‘Jini
Kabula’ na Isabela Mpanda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu na wasanii hao kikizungumza
kilisema, wawili hao kwa sasa wamerudisha urafiki wao kama zamani na
wamemaliza bifu lao kwani walikuwa hawaongei wala kupeana salamu.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliwatafuta, wasikie:
“Kugombana ni kitu cha kawaida hata kama ni ndugu, Isabela ni kama ndugu
yangu tulipishana kauli, tumemaliza tofauti,” alisema Jini Kabula huku
mwenzake akimalizia:
“Binadamu tunapishana na kupatana, tumeshapata, tunaganga yajayo.”
No comments:
Post a Comment