HALI
ya hewa imechafuka kwa wakazi wa eneo la Ubungo-Darajani karibu na
River Side baada ya majambazi kumuua Sista wa Parokia ya Makoka-Mwisho
aliyefahamika kwa jina moja la Kapuli na kisha kumjeruhi dereva wa gari
na kutokomea na mkoba wa marehemu kusikojulikana.
Tukio
hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu leo mchana wakati
sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa
lengo la kununua mahitaji muhimu.
Shuhuda
wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark
Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na
watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na
kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.
Aliongeza
kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele
kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao
waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi
dereva huyo kidoleni.
(HABARI/PICHA: Deogratius Mongela / GPL)
No comments:
Post a Comment