Makala
RIO DE JANEIRO, Brazil
KIULIZA washambuliaji ambao wapo ‘on fire’ kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil, haraka jina la Neymar litatajwa na wengi, staa huyo wa Brazil ameshafunga mabao manne mpaka sasa katika michuano hiyo.
Wachambuzi wa soka wanaamini kijana huyo ‘sharobaro’ anao uwezo wa kutwaa tuzo hiyo na sababu kubwa tatu zinatajwa, ikiwa ni saa chache kabla ya kuliwakilisha taifa lake katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo dhidi ya Chile.
Anaungwa mkono
Neymar alifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Croatia iliyokuwa ya ufunguzi, ilionekana wazi kuwa Wabrazili wote walikuwa nyuma yake, kwani kila alipokuwa akigusa mpira na kuonyesha makali, shangwe zilikuwa kubwa.
Brazil itafika mbali
Brazil haina makali sana lakini inavyozidi kucheza ndivyo inavyoonekana kuwa inaweza kuwa tishio, inaweza kufika hata nusu fainali au fainali, ikiwa hivyo maana yake ni kuwa Neymar atakuwa na muda mzuri wa kufanya kweli.
Unaikumbuka ile penalti ambayo Fred alijiangusha katika mechi dhidi ya Croatia? Picha za marudio za tukio hilo zilionyesha wazi kuwa straika huyo akuvutwa bali alianguka mwenyewe baada ya kuguswa kidogo.
Hivyo, kama wenyeji watapewa penalti kirahisi na vitu vingine kama hivyo, jukumu kubwa la Neymar litakuwani kutenga mpira sehemu inapotakiwa kisha kutazama kipa amesimama wapi na baada ya hapo ni kurusha makombora.
No comments:
Post a Comment