Ali Kiba ameeleza kutopendezwa na maelezo yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Diamond wana ugomvi.
Akiongea na Bongo5 mwimbaji huyo amesema wapo watu ambao hutumia hata akaunti fake za Facebook kwa lengo la kuwagombanisha.
“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya.” Amesema Alikiba
“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe.” Ameongeza.
Katika hatua nyingine, Ali Kiba ameeleza kuwa tayari ameshafanya maandalizi ya video za nyimbo zake Kimasomaso na Mwana Dar es Salaam na kwamba video moja ataifanyia ndani ya nchi na nyingine nje ya nchi.
Chanzo: Bongo5

No comments:
Post a Comment