Monday, August 4, 2014
ALI KIBA: LULU ANAFAA KUWA MKE
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke. Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa? Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.
KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.
KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.
“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi wetu ili azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta ili afunguke).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment