Daktari wa Marekani aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola amewasili nchini humo kutoka Liberia ili kupata matibabu.
Daktari Kent Brantly alisafirishwa kwa ndege maalum hadi katika kambi moja ya kijeshi katika jimbo la Georgia nchini Marekani..Anapewa matibabu akiwa ametengwa katika hospitali moja mjini Atlanta.
Hiki ni kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kutibiwa nchini marekani.
Daktari Jay Verkey ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya maambukizi katika hospitali hiyo amewahahakishia raia kwamba ugonjwa huo ambao hauna tiba,hautasambaa.
Raia mwengine wa Marekani aliyeambukizwa Nancy Writebol anatarajiwa kusafirishwa kutoka Liberia katika siku chache zijazo.
Zaidi ya watu 700 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika eneo la Afrika magharibi ambao una waathiri raia nchini Guinea,Liberia na Sierra Leone.
No comments:
Post a Comment