Wilbert Molandi na Hans Mloli
IMEFAHAMIKA kuwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo amepanga kukitumia kikosi cha pili kwenye michuano ya Kombe la Kagame ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 8, mwaka huu nchini Rwanda.
Gazeti hili limegundua hilo kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, jana.
Katika mazoezi hayo, Maximo alitenga vikosi v
iwili vilivyofundishwa na makocha wanne wa timu hiyo, Maximo yeye alikuwa na Salvatory Edward wakati Leonardo Neiva akiwa na Shadrack Nsajigwa.
Kikosi cha Neiva na Nsajigwa ambacho imeelezwa kuongozana na timu hiyo kwenye michuano hiyo, kiliundwa na vijana waliopandishwa kwenye msimu huu na baadhi ya wakongwe ambao ni Ali Mustapha ‘Barthez’, Omega Seme.
Wengine ni Rajab Zahir, Hussein Javu, Nizar Khalfani, Said Bahanuzi na Pato Ngonyani vijana ni Amosi Adeli, Khamisi Issa, Bensoni Mikaely, Mandela Mgunda, Shabani Idd, Mwinyi Ndimbo, Franky na wengine waliosajiliwa hivi karibuni wakitokea kwenye michuano ya Rolling Stone.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Yanga, kikosi hicho kitaongozwa na Nizar ambaye yeye amepewa unahodha kutokana na uzoefu alionao.
Wakati huohuo, beki wa zamani wa timu hiyo, Shadrack ameweka wazi kuwa amefurahia kuanza majukumu mapya klabuni hapo ambapo atakuwa msaidizi wa Maximo pamoja na kusimamia kikosi cha vijana cha Yanga akisaidiana na Neiva.
No comments:
Post a Comment