Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati
za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya
kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya
uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa
NBC, METL na Star Oils.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu
wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini
hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 kwa ajili ya kampuni
dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na
usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
No comments:
Post a Comment