UPAKO!
Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea katika Tamasha la Matumaini
litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa, Agosti 8, mwaka huu, pamoja na
burudani mbalimbali, waimbaji wa muziki wa Injili watakuwepo kulipamba
tamasha hilo.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman
Maloto alisema kila kitu kimekwenda kwenye mstari na kinachosubiriwa ni
muda ufike, Watanzania wajumuike kwa pamoja uwanjani kushuhudia burudani
zisizo na mfano.
Kwenye muziki wa Injili, Maloto alisema mkongwe wa nyimbo za Injili,
Upendo Nkone ataliongoza jukwaa kwa kuporomosha nyimbo kama Haleluya
Usifiwe, Mwambie Yesu, Unastahili Kuabudiwa, Usinipite Bwana na nyingine
nyingi.
Kama hiyo haitoshi, watakuwepo Martha Mwaipaja anayetamba na wimbo wa
Tusikate Tamaa na Ombi Langu, pia katika kundi hilo wapo Ambwene
Mwasongwe, Angela na Paul Clement.
Katika kuleta raha zaidi, Maloto alisema mgeni rasmi safari hii atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Katika kuleta raha zaidi, Maloto alisema mgeni rasmi safari hii atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
“Dk. Bilal ndiye atakayepuliza kipyenga kuanza kwa mechi kati ya Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga.”
Kwa upande wa Wabunge wa Yanga imefanya usajili wa nguvu kwa
kumchukuwa, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Simba
wamefanikiwa kumsajili, Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa
Pia viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakiwemo mawaziri na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo na kuandika historia kwa pamoja.
Pia viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakiwemo mawaziri na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo na kuandika historia kwa pamoja.
Maloto amesema kutakuwa na mpambano mkali kati ya bondia
anayeshikilia mkanda wa UBO, Thomas Mashali dhidi ya Mada Maugo ambaye
hajawahi kumpiga mwenzake huyo katika pambano lao lilofanyika mara ya
mwisho.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kumuona mkali wa muziki wa
dansi, Khalid Chokoraa akizichapa dhidi ya Said Memba huku mastaa wa
Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’ akizitwanga na Cloud 112.”
Ndondi nyingine za kukata na shoka ni pale Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atakapozichapa ulingoni na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala.
Ndondi nyingine za kukata na shoka ni pale Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atakapozichapa ulingoni na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala.
Maloto aliongeza kuwa kutakuwa na mechi kali za mpira wa miguu ambapo
Azam FC itaumana vikali na Mtibwa Sugar.Kama hiyo haitoshi, Bongo Movie
watakipiga na Bongo Fleva. Akasema burudani haitaishia hapo, kwani
mastaa kibao wa Bongo Fleva watakuwepo kupiga shoo baab’kubwa.
“Tutakuwa na mfalme wa Bongo Fleva, Ali Kiba. Mashabiki wategemee
kusikia nyimbo zake zote kali sambamba na hizi mpya za Kimasomaso na
Mwana.”Mastaa wengine watakaolipamba jukwaa siku hiyo ni pamoja na
Madee, Meninah, Scorpion Girls, R.O.M.A, Nyandu Tozi, Navy Kenzo,
P-Plan, Shilole, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.
Tamasha la Usiku wa Matumaini limedhaminiwa na Vodacom, Pepsi, PSI,
Benki ya Posta, GEPF, Azam TV, E.FM (93.7), Gazeti la Championi, Times
FM (100.5), SYSCORP na Clouds FM/TV.
No comments:
Post a Comment