Mtangazaji
wa Kituo cha Times FM, Hadija Shaibu akikata keki kwenye sherehe ya
kuzaliwa kwake iliyofanyika nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es
Salaam.
Msanii wa filamu Bongo JB, akilishwa kipande cha keki na Dida mara baada ya zoezi la kulishana kuanza.
Rose Ndauka hakuwa nyuma kuonja kipande cha keki kilichokuwa kimeandaliwa kama moja ya ishara ya upendo kwenye sherehe hiyo.
Dida
akitoa neno la shukurani kwa wangeni wake wote waliyohudhuria
kusherekea pamoja naye kwenye siku ya kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia
leo.
USIKU
wa kuamkia leo Mtangazaji wa Kituo Cha Times FM, Hadija Shaibu 'Dida',
alifanikisha kujumuika nyumbani kwake Mwanyamala Manjuju na baadhi ya
ndugu,jamaa na marafiki zake wa karibu katika kusherekea siku ya
kuzaliwa kwake, ambapo alikuwa ameandaa chakula cha usiku,vinywaji vya
kila aina na burudani mbalimbali kutoka kwa marafiki zake wasanii.
HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL.
No comments:
Post a Comment