Imekaa poa sana! Ubuyu kutoka Hong Kong, China
unadai kwamba mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda hivi karibuni
alimfuata Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani
aliyefungwa nchini humo kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kadinda ambaye ni meneja wa Wema
Isaac Sepetu zilidai kwamba katika safari yake nchini humo, alifuatana
na Wema na Petit Man.
“Kadinda amepongezwa sana kwa hatua yake hiyo, kuhusu kama alionana
naye au alichoongea naye, tusubiri arudi maana bado yupo China,” alisema
rafiki wa mmiliki huyo wa lebo za mavazi za Single Button na
Kwachukwachu.
No comments:
Post a Comment