Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu
ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss
Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani.
Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi
karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la
Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili
ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania.
Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa
Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na
mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa
wema aliomtendea Mungu.
“Watu wanaendelea kumsema mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru
Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa
hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu
wanavyomsimanga,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nabii
Yaspi ili kupata uhakika wa mrembo huyo kutinga kanisani kwake ambapo
alikiri ni kweli alikwenda kanisani kwake na ameshampigia maombi kwa
Mungu hivyo atanyakua Taji la Miss World mwaka huu.
Sitti alishiriki shindano hilo tangu ngazi ya vitongoji na kutwaa
Taji la Miss Temeke kabla ya kuibuka kidedea kwenye Miss Tanzania
linalofukuta ambapo kesho (Jumanne), mkurugenzi wa shindano hilo, Hashim
Lundenga anatarajiwa kutoa tamko rasmi.
No comments:
Post a Comment