Na Imelda mtema
Unyama! Dada wa kazi (hausigeli), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi nyumba ya jirani.

Akizungumzia mkasa huo kwa masikitiko makubwa uliojiri hivi karibuni
maeneo hayo, baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la
John alisema kuwa, siku ya tukio hilo alimuona hausigeli huyo akiwa
amemshika mkono mwanaye huku akiwa na majeraha kwenye jicho na kichwani.
Alisema alipomuuliza nini kimetokea, hausigeli huyo alimjibu kuwa mtoto Samwel aligongwa na pikipiki.
John alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa kazi.
John alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa kazi.
“Nilikuwa nashangaa maana kila hausigeli huyo akizungumza kuwa mtoto
amegongwa na pikipiki, mwanangu alikuwa akimnyooshea kidole na kusema
kuwa yeye ndiye amemuumiza,” alisema mzazi huyo.
Mzazi huyo aliendelea kusema kwamba, baada ya kuona hivyo alimshika
mkono mwanaye hadi kwenye nyumba ambayo anafanya kazi msichana huyo huku
mtoto huyo akimuongoza chooni ambapo alikuta damu nyingi zimetapakaa.
Alisema kuwa alipoona hivyo ilibidi amchukue mwanaye na msichana huyo
hadi polisi kwa ajili ya kupata PF-3 kwa ajili ya matibabu.Kwa upande
wake hausigeli alipoulizwa ni kwa nini alifanya kitendo cha kinyama
kiasi hicho alisema kuwa alikuwa akitamani kumtoa jicho mtoto huyo.
“Alisema kuna shetani au roho ilikuwa ikimtuma amng’oe macho mwanangu,” alisema baba huyo.
Baada ya kujieleza, hausigeli huyo alitupwa korokoroni nyuma ya nondo za mahabusu kwa kitendo alichokifanya ambapo hadi gazeti hili linaanua jamvi maeneo hayo alikuwa kwenye Kituo cha Polisi cha Tabata akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment