BINADAMU
tumeumbwa kwa namna tofauti sana, ingawa kibaolojia, wote tuko sawa,
bila kujali kama ni Wahindi, Waarabu, Wazungu, Waafrika, Wachina na
makabila yote, siyo warefu, wafupi, wembamba wala wanene.
Tunatofautiana akili, uwezo wa kuelewa, uwezo wa kukabili changamoto
na hata jinsi ya kuishi kwenye jamii inayotuzunguka. Kuna watu wengine
hawaamini kama wao wako vile walivyo kwa sababu yao wenyewe, bali
wanamsingizia Mungu.
Mungu alituumba wote tukiwa na akili, kinachotokea ni kujiongeza tu,
kwa elimu ya darasani na hata ya mtaani, lakini ukifunua kichwa changu,
utakuta kina kila kitu ambacho kipo kichwani mwa Steve Jobs, yule
bilionea namba mbili duniani.
Ndivyo pia tulivyo hata katika maisha ya uswahilini. Unashangaa
watoto wawili wa kiume wamezaliwa kwa wazazi walewale, lakini staili ya
maisha yao ni tofauti kabisa, mmoja ni mpole na mtanashati, mwingine ni
mtukutu asiyekamatika.
Kuna wengine kutokana na hali ya maisha yao, wanaamini kwamba wao ni
wabaya kiasi kwamba hawawezi kupata wenza wenye maana. Hivi, hebu jaribu
kufanya utafiti wako mwenyewe mdogo. Mchukulie msichana mwenye sura ya
kawaida tu lakini anayeishi katika familia bora anavyokuwa.
Atatumia
uwezo wa wazazi wake kufanya shopping ya maana na atajiremba sana kiasi
kwamba ataonekana ni mrembo kuliko msichana kutoka familia iliyochoka
ambaye ana uzuri wa asili, lakini uwezo wake duni kifedha, unamfanya
ashindwe kujifanyia manjonjo.
Vivyo hivyo kwa wavulana, wapo wenye miili iliyopendwa na akina dada,
lakini kutokana na ufukara wao, wanashindwa kujitokeza mbele ya
wasichana wazuri kwa sababu hawawezi kusikilizwa, hasa katika kipindi
hiki ambacho ni cha hapendwi mtu isipokuwa pochi.
Lakini mvulana mwenye sura isiyovutia, aliyetoka familia bora atavaa
mavazi ya gharama yatakayomfanya aonekane handsome na wadada
watamkimbilia, naye hakika atajiona ni mzuri.
Kitu tunachoweza kujifunza kutokana na hali hii ni kwamba siku hizi mapenzi hayaangalii sana wajihi wa mtu, bali hali yake.
Upande wowote ambao fedha inahusika, ndiyo ambao una nafasi kubwa ya
kupata mapenzi yenye uhakika, wakati upande wa pili kidogo hali huwa
siyo rahisi. Hapa ndipo baadhi yetu tunapokosa ujasiri hadi kujikuta
tunakimbilia kwa binadamu wenzetu, tuliowapa jina la waganga na kuamini
kuwa wanaweza kutusaidia kuwapata wenza!
Wapo ambao maisha yao ya kimapenzi yamewafanya wajione kama wenye
mikosi, wamejikuta wakiamini kwamba wao ni wabaya na kwamba hawana
bahati. Kama wewe ni mmoja wa watu hawa, safu hii ya leo itakuwa ni
nzuri sana kwako.
Wapo baadhi ya ndugu zangu, wake kwa waume wamekuwa wakinipigia simu
na kunieleza jinsi maisha yao ya kimapenzi yalivyotawaliwa na kile
wanachosema kuwa ni mikosi, kwamba kila baada ya muda mfupi, wapenzi wao
ama wanageuza njia au lolote ambalo huliweka penzi lao katika hali ya
sintofahamu.
Kwanza ni lazima tufahamu kwamba katika mapenzi, hakunaga mtu mzuri wala mbaya.
Wengine wanajidanganya kwamba wao ni warembo kuliko wenzao. Hapana,
mapenzi ni hisia. Kila mtu ana hisia na kwa maana hiyo, yeyote anaweza
kumpata mwenza. Kinachotufanya tujione kuwa na mikosi ni kwamba achilia
mbali matatizo yetu ya kibinadamu, lakini pia huenda wenza
tunaowachagua, hawana hisia kwetu. Usidhani urembo wa sura na umbo ni
kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu avutiwe na wewe. Ni zaidi ya hapo.
Ndiyo maana hushangai kwa nini wenzetu wenye ulemavu, uwe wa viungo
au ngozi, mbona na wenyewe wana watu wao? Kama mapenzi yangekuwa siyo
hisia, hawa wasingepata wenzao kwa sababu watu wangeogopa ulemavu wao.
Kuna watu wana magonjwa yao, mtu mwingine anapenda matiti makubwa au
madogo, akimuona mwanamke aliyenayo, hajali, hata kama hana miguu!
Ndiyo maana nimekwambia, acha kujiona mwenye mikosi, isipokuwa tambua
bado hujampata mtu ambaye anaendana na wewe kwa hisia. Ni kujidanganya
kumtafuta kwa waganga wa kienyeji!
Wednesday, October 22, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment