WATU kadhaa
wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye ajali ya
basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar lililopinduka
eneo la kona ya Phantom, Kahama.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na kupinduka.
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.
Taarifa zaidi pamoja na picha za ajali hiyo zitawajia hivi punde.

No comments:
Post a Comment