
Mtuhumiwa Cherif Kouachi (kushoto) na ndugu yake Said Kouachi.
Polisi wakiendesha oparesheni ya kuwakamata watuhumiwa katika
kitongoji cha Croix-Rouge eneo la Reims, kaskazini mwa Ufaransa.
Kikosi maalum cha kupiga vita ugaidi cha Ufaransa kikiwa kazini kuwasaka watuhumiwa.
Mmoja wa askari dhidi ya ugaidi wa Ufaransa kajizatiti kwa kila hali.
Polisi wakilinda jengo moja huko Reims wakati wapelelezi wakiendesha shughuli zao kuhusiana na shambulio hilo la kigaidi.
Askari wapelelezi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo sehemu mbalimbali.
NDUGU wawili na kijana mmoja jana walielezewa kuwa
ndiyo watuhumiwa watatu wanaohusishwa na shambulio la kigaidi jana dhidi
ya jarida lenye kupinga Uislam nchini Ufaransa liitwalo Charlie Hebdo
mjini Paris ambapo watu 12 waliuawa na saba kujeruhiwa.
Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na mhariri mkuu, wachoraji wanne wa vikatuni na polisi wawili.
Inasemekana
sababu ya kuvamiwa kwa ofisi za jarida hilo ni kuchapisha vikatuni
vyenye kukashifu dini ya Kiislam. Washambuliaji hao walitoroka baada ya
shambulio hilo.
Watuhumiwa hao ni Said Kouachi (34), Cherif
Kouachi (32) wote wakazi wa jiji la Paris, ambao ni pamoja na Hamyd
Mourad (18) kutoka mji wa kaskazini-mashariki wa Reims, Ufarransa,
aliyejisalimisha polisi baada ya kuona katika vyombo vya habari alikuwa
anatafutwa.
Hivi sasa polisi wanawatafuta ndugu hao wawili katika eneo la Croix Rouge hulo Reims.
No comments:
Post a Comment