Kyle Jones (31) akiwa na mpenzi wake, Karen, anasema huvutiwa tu na wanawake wanaomzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka.
Huyu ndiye Kyle, kijana mtanashati anayeachwa hoi na penzi la vibibi vizee.
Kyle and Karen wakiwa katika ‘mahaba niue’ walipokutana mara ya kwanza.
Kyle akiwa na mmoja wa ‘magelfrend’ zake wazee.
Nywele, tabasamu na umbo la Karen (kulia) ni baadhi ya vitu vilivyomvutia Kyle.
Kyle akiwa kakolea katika hisia kali na mpenzi wake mzee zaidi aitwaye Marjorie McCool, mwenye umri wa miaka 91.
KYLE JONES wa Pittsburgh, Pennysylvania, nchini
Marekani, aliye na umri wa miaka 31, ameelezea kuvutiwa kwake na
wanawake ambao wanamzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka. Kijana huyo
ameweka wazi kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
hajafanya mawasiliano yoyote ya kimapenzi na mwanamke aliye chini ya
umri wa miaka 60.
Kyle ambaye alifichua hayo jana kipindi maalum cha kituo cha
televisheni cha TLC kiitwacho ‘My Strange Addiction’ (Tamaa Yangu ya
Ajabu), alisema mpenzi wake mzee zaidi wa kike ana umri wa miaka 91.
“Nawapenda wazee wa kike kwa kila kitu. Napenda harufu yao, napenda
kuwa karibu nao na hisia zao,” alisema katika kipindi hicho kijana huyo
ambaye alipokuwa na umri wa miaka 18 alikuwa tayari amepata mpenzi wa
kike aliyekuwa na umri wa miaka 50.
Kyle alianza kuvutiwa na wanawake wazee akingali shuleni ambapo mtu
wa kwanza kumvutia alikuwa ni mwalimu wake aliyekuwa na umri wa miaka 65
wakati huo.
“Nilimpenda kwa nywele zake nyeupe, umbo lake, na kila kitu,” anasema.
No comments:
Post a Comment