Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
8/1/2015.Dar es salaam.
Mfumuko
wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia
4.8 kutoka asilimia 5.8 iliyokuwepo mwezi Novemba kutokana na kupungua
kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Akitoa
taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Taifa leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim
Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula zikiwemo
Mahindi, Unga wa mahindi, mbogamboga, mihogo ,sukari ,Mafuta ya taa,
dizeli, petroli na Simu za kiganjani kumechangia kupunguza mfumuko wa
bei nchini
Amesema
kuwa wastani wa Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwaka mzima kutoka Januari
hadi Desemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 6.1 kutoka asilimia
7.9 uliokuwepo kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2013.
Ameeleza
kuwa Tanzania inaendelea kufanya Vizuri katika nchi za Afrika
Mashariki katika kudhibiti Mfumuko wa bei kwa kuendelea kuchukua hatua
za kudhibiti viashiria vinawezakuchangia kuwepo kwa mfumuko wa bei.
Akitoa ufafanuzi
kuhusu mfumuko wa bei katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki
Kwesigabo amesema kuwa umekuwa na mwelekeo unaofanana, Kenya ukipungua
na kufikia asilimia 6.02 mwezi Desemba kutoka 6.09 za mwezi Novemba na
Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.1 za
mwezi Novemba, 2014.
Aidha,
amesema mwenendo wa Fahirisi za bei ambacho ni kipimo kinachotumika
kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini
katika kipindi cha mwezi Desemba 2014 amesema kuwa Fahirisi hizo
zimeonyesha kuongezeka hadi kufikia150.92 kutoka 150.54 za mwezi Novemba
2014.
Amefafanua
kuwa kuongezeka kwa Fahirisi hizo kunatokana na kuongezeka kwa bei za
bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo mchele, unga wa
mahindi, samaki, matunda jamii ya machungwa, mbogamboga, mavazi ya
wanaume na wanawake na viatu vya wanaume.
Kwa
upande wake Meneja Utafiti wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Bw.
Johnson Nyella ameeleza kuwa kuendelea kupungua kwa Mfumuko wa Bei
nchini kunatokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali
kupitia Benki hiyo kwa kuangalia utekelezaji wa Sera na Mipango ya
maendeleo.
Amesema kuwa katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na utulivu wa Uchumi kwa
kipindi kirefu, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikifuatilia mwenendo wa
bei katika Soko la Dunia, bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini na
ufuatiliaji wa mwenendo wa uchumi wa nchi zinazoizunguka Tanzania.
Amesema malengo ya muda mrefu ya Benki kuu ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa Mfumuko wa bei unapungua na kufikia asulimia 5.
No comments:
Post a Comment