Shirika la misaada Oxfam limetoa
wito wa kutolewa kwa msaada wa thamani ya mamilioni ya dola kusaidia
nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na Ebola, mradi huu wa msaada
unaitwa Marshall Plan
Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola, wengi wao nchini Sierra Leone,Guinea na Liberia.Mradi wa Marshall ulitumika baada ya vita ya pili ya Dunia kwa ajili ya kuwanusuru waathirika barani Ulaya.
Oxfam imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuridhia mpango wa utoaji misaada kutoka kwa nchi tajiri.
Shirika hilo limesema msaada wa fedha unahitajika katika maeneo matatu-kuchangia pesa kwa Familia za waaathirika wa Ebola, kuwekeza katika kazi pia kusaidia kutoa elimu kuhusu maswala ya kiafya, elimu na usafi.
Utafiti umebaini kuwa asilimia 60 ya Watu waishio kwenye meaeneo yaliyoathirika wanadai kuwa hawajapata chakula cha kutosha kwa kipindi cha juma moja lililopita sababu kubwa ikilezwa kuwa kushuka kwa kipato na kuoanda kwa gharama za chakula.
Nayo Bank ya dunia imekisia kuwa takriban 180,000 wamepoteza kazi zao nchini Sierra Leone tangu kuanza kwa ugonjwa huo, huku wengine wanaotunza familia zao nchini Liberia nao wakipoteza ajira.
No comments:
Post a Comment