Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akisalimiana na
Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara,
Michael Msongazila mara baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
Kwaya
ya vijana ya mara ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za
mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani
Tarime mkoani Mara.
Mgeni
rasmi Mh. Kabaka, Bw. Alvaro Rodriguez na SSP. Simon Mrashani
wakishiriki kucheza wimbo maalum unaohamasisha kukataza vitendo vya uovu
vya Ukeketaji kwa watoto wa kike wakati wa mahafali hayo.
Meza kuu ikitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
Mkurugenzi
wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM), Tarime, mkoani
Mara, Sista Germaine Baibika akimkaribisha mgeni rasmi pamoja wageni
waalikwa kwenye sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa
msimu wa ukeketaji.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifurahi jambo na
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye
sherehe za mahafali hayo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizungumza kwenye
sherehe za mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa
ukeketaji.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa
salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za mahafali sita ya mabinti
waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bw. John Henjewele akitoa salamu kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mahafali ya sita ya kituo cha
kupambana na ukeketaji cha kijiji cha Masanga (TFGM) cha wilayani
Tarime, mkoani Mara.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt Natalia Kanem, akizungumza kwenye sherehe hizo.
Kaimu
kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya SSP. Simon
Mrashani akieleza jinsi jeshi la polisi linavyoshiriki katika kupambana
na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia likiwemo suala la kesi za
ukeketaji ambapo pia alitoa takwimu za kesi zilizoripotiwa kituoni mpaka
sasa ni 141, huku 80 zikiwa Mahakamani na 20 zimetolewa hukumu.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe
za mahafali hayo.
Wahitimu
37 wakila kiapo cha kutokubali kutoshiriki kukeketwa na kuwa mabalozi
wazuri kwenye jamii zao katika kuelemisha madhara ya ukeketaji kwa
wanaoendeleza mila na tamaduni hizo pindi warudipo majumbani.
Mratibu wa kituo cha TFGM
na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha
Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga
akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya
sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).
Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa
Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine
Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa
sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa
ukeketaji.
Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu
mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala
ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo
mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na
kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la
kuendeleza mila.
“Hii sio mila” anasema sista Germaine na
kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au
kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima
ipigwe vita.
Alisema serikali isiache kuwatetea
mabinti hao kwa dai la kuwa hiyo ni mila kwa kuwa wanaofanyiwa vitendo
hivyo hulazimishwa na haifanyiki kwa ridhaa yao.
Alisema wapo mabinti walioletwa na wazazi wao kuepushwa na janga hilo, wapo waliotoroka kwa wazazi wao na wapo walioletwa katika kituo hicho na polisi kutoka makwao.
Mafunzo hayo ya mwezi mmoja yamelenga kukabiliana na msimu wa ukeketaji ambao sisita huyo alisema mwaka jana ulianza mapema Novemba na unaendelea hadi mwaka huu wakati kimila mwaka huu si wa ukeketaji.
Kwa mujibu wa mila za Kikuria ukeketaji hufanyika katika mwaka unaogawanyika, mwaka 2015 haugawanyiki.
Mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwatoa mabinti wa kisasa wenye mwelekeo wa maisha yenye hali bora mabinti wanaofika hapo huwa hawataki kukeketwa na ndio maana mwaka huu walipata tatizo la binti mmoja kuzimia wakati alipomuona baba yake katika maeneo ya kituo hicho.
Alisema wapo wazazi wakorofi wanaokuja kudai watoto wao lakini pia ipo jamii korofi inayotumia ubabe baada ya wasichana hao kutoka hapo wanakeketwa kwa lazima.
Katika hafla hiyo iliyoendeshwa na masista wa shirika la Daughters of Charity of St. Vincent De Paul, Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka aliwapongeza wasichana hao na kuwataka kuwa mfano katika jamii na kutekeleza wajibu wao.
Alisema wamekuwa mabinti wa kisasa kwa kukataa ukeketaji na hivyo wao wanastahili kuwa walimu kwa wenzao.
Aidha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amewataka mabinti hao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na kuwa chanzo cha kubadili kizazi kijacho.
Alisema wamesimama madhubuti kupinga mila potofu na uonevu na kusema kwa kitendo chao wamewafanya wengine kuwaiga na kubadilika.
Alisema ukeketaji ni mila potofu na kusema kwa msaada wa shirika la Umoja wa mataifa la Mpango wa familia (UNFPA) na taasisi nyingine zinazopambana na ukeketaji kwa kipindi cha miaka saba wamefanikiwa kuwoakoa wasichana 2001 wasikeketwe.
Aidha mabinti hao wameokolewa dhidi ya ndoa za utotoni, ujauzito wa mapema na kushindwa kuendelea na masomo.
Katika sherehe hizo ambapo pia askofu wa Musoma alikuwepo na viongozi wengine wa kiserikali pia Ngariba walioacha kazi hiyo walikuwepo kuelezea ubaya wa mila hiyo.
Suala la ukeketaji ni kitu cha kawaida katika mikoa ya Manyara 71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% na Mara 40%.
Viongozi waliopata muda wa kuzungumza walisema kwamba ukeketaji unatakiwa kukomeshwa mara moja kwani ni tatizo si tu kwa jamii bali kwa wale ambao wanafanyiwa kisaikolojia na kitabibu.
Moja ya kazi inayoifanywa na kituo cha Masanga ni ushauri wa kisaikolojia kutokana na wasichana wengi kufika hapo wakiwa na matatizo makubwa ya magonjwa na hasa msongo wa mawazo.
Katika risala yao mabinti hao wameitaka serikali kufanyakazi yake kukabiliana na ubabe unaofanywa na viongozi wa kimila wa kuwalazimisha kukeketwa hata msimu unapokuwa umepita.
Mabinti hao ambao wengi wametoka shule ya msingi na sekondari wameweza kuwekwa hapo kwa msaada wa UNFPA ambao wametoa hela kupitia Children’s Dignity Fund (CDF), .Wafadhili wengine ni Daughters of Charity of St. Vincent Du Paul, na Askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Musoma, Michael Msongazila

No comments:
Post a Comment