Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Wolper’ akipozi.
Akizungumza na Amani, Wolper alisema ameamua kujikita huko kwa sababu
ameona Bongo Movie hakuna maendeleo zaidi ya umbeya na hata soko la
filamu linazidi kushuka.“Mimi ni msanii wa muda mrefu sana na kwa kazi
ambazo tayari nimeshazifanya tangu kipindi hicho mpaka sasa naona tasnia
haina maendeleo bali wamejaa masnichi tu yaani umbeyaumbeya tu.”“Ni bora niwe fundi nguo ili kuepukana na manenomaneno yanayoendelea na mpaka sasa hivi tayari nimeshaanza kujifunza kushona nguo na nina imani nitakuwa fundi mzuri tu kuliko kutegemea kazi ambayo haina masilahi,” alisema
No comments:
Post a Comment