HATIMAYE ila siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapendanao wote ‘Valentine’s Day’ imefika ambapo leo, Februari 14, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar kutafuka moshi wa burudani kutoka kwa wakali wa mapenzi, Christian Bella ‘Obama’ pamoja na Mfalme Mzee Yusuf.
Mkali wa masauti, Christian Bella ‘Obama’.
Good newz kwa wapendanao ni kwamba mkali wa masauti, Christian Bella
‘Obama’ atazindua ngoma yake mpya ya mapenzi kwa mara ya kwanza
inayojulikana kama Nashindwa ikiwa ni zawadi maalum kwa wapendanao wote
watakaofika huku Mzee Yusuf akiendeleza malavidavi.Katika makala haya, yanabainisha utamu zaidi utakaopatikana usiku wa leo.
WAKALI WA BENDI
Haina kupepesa kuwa upande wa muziki wa Dansi, bendi inayobamba kwa sasa kwa kufanya shoo kibao za kufa mtu ni Malaika Music iliyo chini ya Christian Bella.Kuonyesha ni usiku spesho kwa wapendanao, Malaika Music watahakikisha wanawapagawisha wapendanao wote kwa kuimba na kucheza nyimbo zao zote kali za mapenzi kwa staili ya Kizaire na Kibongo.
Nalo kundi linalotikisa kunako miondoko ya Taarab, Jahazi Modern litatanda jukwaa zima la Dar Live likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf.Jahazi watakuwa na wakali kama Leila, Mishi, Fatuma Mcharuko, Mwansiti, Amigo na wengine kibao wakiwapa raha za Kipwani wapendanao.
RED CARPET
Mbali na kuwepo kwa zawadi maalum kwa kapo itakayotoka bomba zaidi. Wapendanao wote watapata fursa ya kupiga picha ‘red carpet’ na wakali watakaotumbuiza, Bella pamoja na Mzee Yusuf.
WAKALI WA MAPENZI
Je unajua wakali wa nyimbo za mapenzi wanapokutana pamoja nini kinatokea? Basi leo Dar Live, Mfalme Mzee Yusuf na Jahazi wataanza kwa kulitetemesha jukwaa kwa nyimbo zao kali zote za mapenzi.
Miongoni mwa nyimbo zitakazofunika ni Tiba ya Mapenzi, Wapendanao, My Valentine, Mpenzi Chocolate pamoja na wimbo mpya ambao ni habari nyingine kwa sasa wa Mahaba Niue.
Bella naye atapanda na Malaika kuonyesha kuwa ni hatari kwa nyimbo za mapenzi kwa kuuzindua wimbo wake mpya wa Nashindwa sambamba na kupiga ngoma zake zote kali kama vile Safari Siyo Kifo, Msaliti, Nakuhitaji, Yako Wapi Mapenzi pamoja na wimbo uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
SAPRAIZ KIBAO
Umeshawahi kubadilishana namba za simu na mastaa? Basi kwa mara ya kwanza Bella atabadilishana namba za simu na wapendanao wote sambamba na kuzungumza nao mawili matatu.Nafasi nyingine ambayo ni nadra kuipata kwa staa yoyote itatokea leo, ambapo mastaa kibao wakiongozwa na Bella watajumuika na wapendanao kupata vyakula mbalimbali, nyama choma, vinywaji na vingine vingi vitakavyokuwepo ukumbini hapo.
Mfalme Mzee Yusuf.
BELLA KUFUNIKA JUKWAABella amewahakikishia wapendanao wote watakaofika watashangaa historia atakayoiandika usiku wa leo.“Siyo kama najisifia! Hapana, ila ukizungumzia kati ya wasanii wote Bongo iwe ni wa Taarab, Dansi, Bongo Fleva, Vigodoro ama muziki wowote, hakuna msanii ambaye anafunika jukwaani kama mimi.
Nikipanda tu jukwaani nasomba mashabiki wote, hata kama walikuwa wamelala, wapo mbali wote wanahamia kwangu na kuimba nao pamoja. Wapendanao wajiandae kwa kufanya maajabu ya aina yake jukwaani.”
***
MSANII AJIVUNIA KUFANYA KAZI NA NATURE
Stori: Mikito Nusunusu
BWA’MDOGO anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Hassan Ridhiwan ‘Perfect Rymes’ amefunguka kuwa anajifunia kufanya kazi na legendari wa muziki huo, Juma Kassim ‘Nature’ kwani ni wachache sana wanaoweza kupata bahati hiyo.
Akizunguza na Mikito Nusunusu, Perfect Rymes alisema kitendo cha yeye kufanya wimbo wa Sindanganyiki katika Studio Uprise Music kwake ni chachu ya kufanya vizuri hivyo atazidi kukaza ili atusue.
“Muziki unahitaji kupatambana ili uweze kufanikiwa, kuanza kufanya kazi na mkongwe kama Nature ni hatua nzuri kwangu, niwaombe mashabiki wanipe sapoti naamini nitatoboa,” alisema Perfect Rymes.
***
KEISHA: INAUMA WANATUUA KAMA KUKU!
Stori: Laurent Samatta
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hadija Shaban ‘Keisha’, amefunguka kuwa anaumia kuona watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanaendelea kuuawa kama kuku wakati kila siku elimu inatolewa.
Keisha ametumia sana kipaji chake kufikisha ujumbe kukemea mauaji hayo lakini anashindwa kuelewa ni kwa nini kesi za mauaji ya albino zimekuwa zikicheleweshwa.
“Tunaumia sana hiki ni kilio chetu cha muda mrefu sana lakini bado mambo yanaendelea, nakosa hata imani na mamlaka zinazohusika,” alisema Keisha.
No comments:
Post a Comment