Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii
ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel
Nyalandu na mkewe Faraja Kotta wamejibu tetesi kuwa mheshimiwa alikuwa
na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
Grayson.
Kwa mujibu wa Nyalandu ambaye ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais mwaka huu, hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwa kuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu.
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina dili kabisa.
“Hata anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza.
“Nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na
tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunt Ezekiel
katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndiyo hiyohiyo siku nimemuona,
nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.“Tumekutana naye akiwa mwalikwa pamoja na maDJ wengine wa Bongo Fleva katika tukio lenye watu wengi ambao ni Watanzania waishio Marekani.
“Nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwa hiyo kwanza katika hali hiyo ya kuwa Amerika (Marekani) atakuwa aliniona kwa saa moja kwenye ule mkutano.
“Lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye,” alisema Nyalandu pembeni akiwa na mkewe.
No comments:
Post a Comment