ALIYEMREKODI EDZEN VIDEO YA UTUPU YAMKUTA
JESHI la polisi jijini Dar limemkamata binti anayefahamika kwa jina
la Moza kwa kosa la kudaiwa kumdhalilisha Mtangazaji wa Runinga ya TV1,
Ezden Jumanne ambapo anatarajiwa kuburuzwa mahakamani muda wowote baada
ya uchunguzi kukamilika.
Moza anayedaiwa kumrekodi Ezden video ya utupu.
Moza ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo kisha
kuachwa, anadaiwa kumrekodi video ya utupu Ezden kipindi walipokuwa
kwenye uhusiano mzuri kisha kuisambaza mitandaoni walipogombana.
Chanzo makini kimedai kuwa, Moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu
katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar kufuatia msako mdogo
uliofanywa na polisi saa chache baada ya mrembo huyo kuvujisha video
hiyo.
“Wameshamtaiti
pale Oysterbay, wanakamilisha tu taratibu za ushahidi kisha anaburuzwa
mahakamani muda wowote kuanzia sasa,” kilisema chanzo chetu, juzi
Jumatano. Moza amedaiwa kuiachia video hiyo mapema wiki hii kutokana na
chuki za kuona Ezden ana mwanamke mwingine hivyo akaona akivujisha video
hiyo atakuwa amemkomoa mtangazaji huyo kijana aliyewahi kuwa mume wa
Mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’.
Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Jumanne.
Akizungumzia sakata hilo, Ezden alisema yeye ni mtu anayejiheshimu,
anajitambua hivyo kitendo cha mwanamke huyo kumrekodi video hiyo
hakikuwa cha kiungwana.
“Hakunitendea haki, Nimeshalifikisha suala
hili polisi, taratibu za kipolisi zikikamilika anaburuzwa mahakamani,”
alisema Edzen.
No comments:
Post a Comment