Mkurugenzi
wa Kampuni ya Serengeti Brewers Ltd, Steve Gannon (kushoto) akimpa
mkono wa pongezi Linah (katikati) baada ya kukubali kusaini mkataba wa
kuwa Balozi wa Jebel. Kulia ni meneja wa Linah, Tonny Akwesa,
akishuhudia makabidhiano hayo.
Linah
(kulia) akisaini mkataba huo na Mkurugenzi wa Serengeti, Steve Gannon,
ndani ya ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi kuu za kampuni hiyo
Temeke, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Linah na Mkurugenzi wa Serengeti Gannon wakionyesha kinywaji cha Jebel.
Steve Gannon akiangalia T-shirt yenye nembo ya kinywaji hicho mara baada ya kusainiwa na Linah.
…Akionyesha T-shirt hiyo baada ya kusainiwa na Linah.
Linah akiongea jambo kwa waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba.
Mkurugenzi
Masoko wa Serengeti, Cescar Mloka (wa pili kulia), akifurahia jambo
akiwa ameshikilia kinywaji hicho na Linah. Wengine ni Tonny Akwesa na
Steve Gannon.
Linah akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti.
…Akitambulishwa kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Serengeti akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumtambulisha Linah.
Linah akiwa na wafanyakazi wa Serengeti.
MSANII kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania
(THT) Estelinah Sanga ‘Linah’, leo ameingia mkataba na Kampuni ya
Serengeti Breweries Ltd, kupitia kinywaji chake cha Jebel.
Akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba huo, mkurugenzi wa
kampuni hiyo, Steve Gannon, alisema wameamua kumpatia ubalozi wa
kinywaji hicho Linah kufuatia uwezo wake mkubwa katika kuwashawishi
wateja wao, na pia hiyo ni njia mojawapo ya kusapoti kipaji chake na
itakuwa pia njia ya kushirikiana na wasanii wa Tanzania kwa kila kitu.
“Kampuni yetu imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Linah ikiwa njia ya
kutambua sanaa ya muziki Tanzania. Serengeti Brewers Ltd kupitia
kinywaji chetu cha Jebel, tumefurahishwa na uwezo wa Linah hivyo
tunaamini kupitia kwake tutaweza kupata manufaa makubwa ya kutangaza
kinywaji chetu cha Jebel,” alisema na kuongeza:
“Tunatarajia kuanza naye kazi rasmi kwa kutengeneza video ya wimbo
wake mpya ambayo ataifanyia katika nchi ya Kenya na Afrika Kusini.
Video hiyo itakuwa chini yetu, ila mkataba huu utambulike kwamba
tunaanza na mwaka mmoja ingawa utakuwa endelevu zaidi.”
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
No comments:
Post a Comment