KAULI ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuwa kiasi cha shilingi milioni 10 alizotoa haraka kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow alizowekewa na mfanyabiashara James Rugemalila zilikuwa ni za mboga, zimewakera mastaa kiasi cha kumshambulia na kumuita mwenye dharau iliyopitiliza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar kwa njia ya simu, walisema fedha hizo ni nyingi ambazo zingeweza kuwasaidia wagonjwa mbalimbali, uchimbaji wa visima, kusaidia elimu, chakula kwa familia zisizojiweza na makundi mengi yenye uhitaji.
No comments:
Post a Comment