MSANII wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye alitumia muda wake mwingi katika maisha yake ya ujana kwa kujirusha, amesema sasa yatosha na kwamba huu ni muda muafaka kutengeneza maisha yake ya baadaye.
Akipiga stori na gazeti hili, Nisha alisema kwa sasa ameamua kuachana na maisha hayo kwa vile umri unakwenda na ni vyema akatumia muda uliobaki kufikiria kuhusu maendeleo yake, hasa yajayo.
“Naogopa sana kuja kujutia ujana wangu uzeeni, maana unaambiwa fainali uzeeni, kama ni starehe nimeshafanya nyingi sana, sasa hivi nimeamua kuachana nazo maana sioni faida yake,” alisema Nisha.
No comments:
Post a Comment