Michael Sangu ‘Mike’.
Richard BukosSIKU chache baada ya mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ kumwagana na mkewe mwigizaji Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, amedaiwa kumnasa staa mwingine wa filamu, Halima Yahaya ‘Davina’ kwa kuwa naye karibu kiasi cha kuibua maswali.
Staa wa filamu, Halima Yahaya ‘Davina’.
Alipoulizwa Davina kama ameridhia kauli ya kuwa ‘misezi’ wa Mike, alikataa katakata na kumpa ‘makavu’ laivu staa huyo:“Kamwe siwezi kutembea na Mike na haiwezi kutokea hadi nakufa.
Kama anasema hivyo kwa lengo la kutafuta kiki aseme! Asitake kunigombanisha na rafiki yangu Thea (mke wa Mike waliyemwagana) tunaheshimiana sana, tena akiendelea kuropoka ujinga huo atanijua mimi ni nani. Anikome.”
No comments:
Post a Comment