Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazosababisha wanaume kutoka nje ya uhusiano wao wa kimapenzi.
Hulka(Tabia)
Wanaume wengine wana tabia tu ya kupenda kuwa na wapenzi wengi, hawaridhiki na mwanamke mmoja. Hawana hofu ya Mungu na hili hulifanya hata kama hakuna ugomvi wowote nyumbani. Kwao, kile demu aliyependeza anayekatiza mbele yao wanamtamani.
2. Kutojiachia faragha
Labda hili wengi hawapendi kuliweka wazi. Wanawake ni watu wa aibu, hawapendi kujiachia kwa kuonesha wanachojua chumbani, wanaamini kwa kufanya hivyo wataonekana wahuni. Kwa sababu hiyo hupenda kushiriki tendo ‘kistaarabu’ na heshima, tena hivyo hivyo kila siku, inachosha. Mwanaume anaona bora ‘akatesti’ ladha nyingine nje.
Wanaume wengi hasa hawa vijana wa sasa wanafuata mkumbo wa marafiki kwa kutaka kufanana nao. Wakiona kila kwenye tukio flani wenzao wamekuja na ‘vitu vipya’ nao hutamani kuwa hivyo, hivyo kujikuta wakichepuka. Baadhi yao hujisifu kijinga kuwa hata wazazi wao walikuwa viwembe hivyo wamerithi.
4. Umaarufu
Baadhi ya wanaume hudhani kuwa kuchepuka ni sifa inayowapa umaarufu kwa kuonekana wao ni hodari. Wengine hutaka kuonesha kuwa wao ni vidume vya mbegu. Ingawa kimsingi inawaondolea heshima kwa kutongoza kila mwanamke anayekuwa mbele yao, lakini kwao ni fahari ya kujitapa nayo mbele ya wenzake.
5. Mazingira
Wakati mwingine wanaume huponzwa na mazingira wanayoishi au anayokuwemo. Akienda safari, kwa mfano aina ya marafiki na matendo yao wanapokuwa baa au sehemu ya starehe yanaweza kumgeuza juu ya mwenendo wake, hasa kwa wanawake. Huogopa kuonekana ‘mshamba’.
No comments:
Post a Comment