Ugua pole! Hali ya mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ni ya kumwachia Mungu kwani bado ni tete na watu wamekuwa wakimiminika kwa ajili ya kumuona katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar alikolazwa.
Mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ akiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar alikolazwa.
Ijumaa Wikienda lilitia maguu kwenye hospitali hiyo na kufanikiwa
kumuona Banza ambaye kwa wakati huo alikuwa amezungukwa na watu
mbalimbali, wakiwemo wanamuziki wenzake wa dansi wengi wakiwa ni wale wa
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
“Yaani inahuzunisha kwani huyu siyo yule Banza tuliyemzoea, hali yake hii ni ya kumwachia Mungu tu kwani ndiye anayejua kila tatizo linalomtokea binadamu litaondokaje, kikubwa ni kuendelea kumuombea tu maana hatua aliyopo siyo nzuri, ni Mungu tu aweke mkono wake,” alisema mmoja wa wanamuziki ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini.
Naye kaka wa Banza, Hamis Masanja alisema waliamua kumpeleka hospitali kutokana na hali yake kuwa mbaya ambapo Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka akiwa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) walifika nyumbani kwa ajili ya kumjulia hali ndipo wakaafikiana kumpeleka hospitali.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.
Banza akiwa na afya yake jukwaani.
KUTOKA KWA MHARIRIIjumaa Wikienda linaungana na Watanzania kumuombea Banza Mungu amponye kwa neno lake kutoka kwenye Kitabu cha Yeremia 30:17 linalosema: “Kwa maana nitakurudishia afya nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana kwa sababu wamekuita mwenye kutupwa wakisema ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.”
No comments:
Post a Comment