MSANII maarufu wa filamu hapa nchini, Jacob Steven ‘JB’,
amewataka wasanii wakongwe na wenye majina kufuata nyayo za chipukizi
wasio na majina ili waweze kumudu soko la sasa.
JB, aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano na kipindi cha Take
One cha Clouds FM kuwa, wasanii wa zamani wenye majina, wamebakia kubaki
na majina yao na kushindwa kuendana na chipukizi ambao wanakuja kwa
kasi na kutikisa tasnia hiyo.
Aliwataja baadhi ya wasanii ambao wanamsikitisha kupotea katika ‘game’
licha ya kuwa na majina makubwa kuwa ni Wema Sepetu, Irene Uwoya,
Blandina Chagula ‘Johari’ pamoja na Aunt Ezekiel.
Alisema wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu na kushindwa kuendana
na hali halisi ya sasa na kuwa wakati umebadilika, huku akiwashauri
kama wanahitaji kutoka, wanatakiwa kwenda na wakati wa sasa na kufanya
kazi pamoja na chipukizi ambao wanakuja kwa kasi na kuwazidi wao na
ukongwe wao.
“Mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada zetu wamepotea na kubaki
na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka kwa sasa, waendane na
mazingira ya sasa,” alisema.
Alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi wasanii hao wanaigiza, yeye
alikuwa akicheza kama baba na kutokana na juhudi zake za hali na mali,
ndiyo sababu ya kufikia alipo sasa na kujitegemea mwenyewe katika sanaa.
“Mimi kusema kweli nilikuwa kila filamu naigiza kama baba, lakini
nikawa najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini na ndiyo maana
nikajichanganya na nimetoka,” alisema JB.
No comments:
Post a Comment