MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa
kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata
matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na
madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu
lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama
na hana Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni
alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika
Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali
kwenye kanisa hilo.
“Namshukuru
Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi
sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam.
Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu
wanatafsiri kuwa nimeokoka.“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka
wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri
yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.
Credit: GLP
No comments:
Post a Comment