IKIWA
imesalia siku moja kuelekea Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8,
katika Uwanja wa Taifa, diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ ametupa kijembe kwa staa wa Nigeria aliyekuja kukinukisha
Bongo, Yemi Alade kuwa amekuja kufia ugenini.
Diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na Risasi Vibes, Shilole anayetamba na ngoma ya
Namchukua, alijibu tambo za Yemi ambaye alimtambia kuwa amekuja Bongo
kumteketeza.
“Yemi amekuja kukutana na balaa la
mwaka.Siwezi kukubali kuiaibisha nchi yangu kwa kufunikwa na yeye.
Lazima nimuoneshe jeuri anitambue mimi ni nani. Jeshi langu
limeshajipanga na niseme tu kuwa kaja kuteketezwa Bongo,” alisema
Shilole.
Yemi Alade.
Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kufanyika keshokutwa huku
burudani kibao zikitegemewa kutawala uwanjani hapo kama vile, ndondi,
muziki wa Injili, soka na mengine kibao.
No comments:
Post a Comment