Kamanda wa Polisi Kanda Maalum – Dar es Salaam Kamanda Suleiman Kova
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na mafanikio mengine
limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa wizi kwenye mashine za ATM za benki
mbali mbali.
Akitoa
taarifa ya Jeshi hilo leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum – Dar es
Salaam Kamanda Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo Gode Pendacowsk
mwenye umri wa miaka 28 raia wa Makidonia, amekamatwa kwenye hoteli ya
Lamada akiwa na vifaa mbali mbali anavyofanyia uhalifu pamoja na laptop
5.
Katika
hatua nyingine Kamada Kova amesema Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata
bunduki moja aina ya Short Gun Greener na risasi 5 na pia Bastola 5
pamoja Magari 18 jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti.
Amesema
katika tukio linguine polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamefanikiwa
kukamata mifuko 280 ya Mbolea ya Urea mali ya kampuni ya Nyombo
Investment ya nchini Zambia inayokadiriwa kuwa na nathamani ya shilingi
Milioni 48 za Tanzania.
Aidha
kamanda Kova amesema Jeshi hilo pia limekamata noti za Tanzania na Dola
za Marekani bandia zenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni
Thalathini na Tano na Laki Sita (35,600,000/-).
No comments:
Post a Comment