![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxqse68laZP3ab6iZNDkbclZkxTedN-7oEzlsQOekqIFQK0K4CM5vxgKrs91blS_PWWyCGDJo8XOmzDeR8JJv_2kXnbC_nk9hMkY9OXkY6S58In5GzOFnLMQMDzYMMTFt1gi0uyri4ofA0/s640/6924113.jpg)
Kufuatia
Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya
Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha
kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande
zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT)
yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
- Amri
hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012
yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi
amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja
na;
- Iwapo
mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni
makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza
maisha n.k
- Wajibu
maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta
ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha
Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu
zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi
(Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
- Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
- Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa
misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na
wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.
No comments:
Post a Comment