Awali ya yote huyu mtoto na dada
yake wa miaka nane na aunty yake waliamua kufunga safari kwenda kwenye
zoo kama kutalii tu.Kufika kule wakalipia na kufata taratibu zote za
kuingia humo.Wakawa wanatembea wenyewe bila mtu wa kuwaongoza.Aunty
waliyekuwa nae ambae ni mkubwa akawa ameenda chooni kujisaidia.
Huyu mtoto ni mtundu sana akawa
ameona simba yupo kwenye cage akaenda akafungua mlango akawa anataka
kumshika simba.Mwenyewe anasema alikuwa anataka kumshika kidevu,usoni na
kichwani.Ndio simba kumparua kama unavyomuona pichani.Akaja dada mtu
mwenye miaka nane akawa anamvuta mkono kumuokoa huku akipiga
kelele.Kelele zikamfikia baba mwenye asili ya kiasia ndio kuja mbio
kumpiga simba mawe simba akarudi nyuma na kumtoa mtoto.
Baada ya hapo wakampeleka
hospitali kwa matibabu na mpaka sasa anaendelea na matibabu
nyumbani.Malalamiko yao ni kwa nini zoo yao haina ulinzi wa kina kwa
watu wanaoenda hapo?toka mtoto wao amejeruhiwa na simba wamiliki hao
hawajawahi hata kwenda kumjulia hali mtoto wao.
No comments:
Post a Comment