EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, June 14, 2012

MATUKIO BORA 4 NDANI YA GAZETI LA AMANI LA LEO

                 BABA: HAKUNA HAJA YA KUKARABATI KABURI LA KANUMBA

 
Na Gladness Mallya
BABA mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa (pichani) amefunguka kuwa hajui kama kuna haja ya kulijenga kaburi la mwanaye tena kwa kuwa wasanii wenzake walishalikarabati.
Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni mama Kanumba, Flora Mtegoa kutaka baba huyo aulizwe kuhusu suala la kujenga kaburi hilo ili liwe katika hali ya kuridhisha badala ya kukaa na kushindania mali alizoziacha Kanumba.
Baada ya kusikiliza maneno ya mama huyo, paparazi wetu alimtafuta baba Kanumba kwa njia ya simu ambapo alifunguka:
“Haa! Kaburi la Kanumba si limeshakarabatiwa na wasanii wenzake, haina haja ya kulijenga tena labda baadaye baada ya kumaliza mambo ya mirathi kwani kwa sasa ndiyo suala muhimu zaidi.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------

JACK DUSTAN AWEKWA KINYUMBA HOTELINI

Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’.
Na Gladness Mallya
MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’ anadaiwa kuwekwa kinyumba hotelini kwa muda wa wiki moja.
Kikizungumza chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu na 

Jack kilisema kuwa mwanadada huyo aliwekwa katika Hoteli ya Danfrense iliyopo maeneo ya Sinza White Inn, Dar ambapo alikaa na mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina anayeishi nchini Denmark.
“Yaani Jack alikaa hotelini kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya huyo mwanaume wake, naona huyo ndiyo anampa mkwanja ‘so’ yupo tayari kwa lolote,” kilisema chanzo.
Jack alipopatikana alifunguka: “Ni kweli nimekaa hotelini na mwanaume wangu anayeishi Denmark, siwezi kumtaja, alikuja kwa ajili yangu. Pia siwezi kusema ni mchumba wangu kwa sababu bado hajajitambulisha kwetu lakini naweza kusema ni mpenzi wangu tu na ameshaondoka.”
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------
                                     NANI FREEMASON NANI SIYO?



Na Mwandishi Wetu
HALI ya nchi ya Tanzania ni tete kwa sasa, imani ya Freemason inachukua nafasi ya kutajwa kwenye vinywa vya wananchi kila kukicha na kuwafanya wengine washindwe kufanya kazi mazungumzo yakiwa ni imani hiyo yenye utata, Amani limebaini.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa, kwa sasa, kwenye maeneo mbalimbali ya kazi za kila siku, habari kuhusu Freemason inachukua asilimia 75 ya mazungumzo yote kwa siku.
Mbaya zaidi, viongozi wa kisiasa, mastaa wa fani mbalimbali, wachungaji, mashehe, mapedeshee na wafanyabiashara wakubwa wanatajwa kuwa ni waumini wa imani hiyo bila wao wenyewe kuweka wazi jambo hilo.
kigezo kikubwa
Uchunguzi zaidi ukabaini kuwa, kigezo kikubwa kinachotumika kwa sasa kuwataja watu hao kuwa ni Freemason ni pamoja na mvuto katika jamii, utajiri mkubwa, hasa ule wa harakaharaka na ambao akili za watu hazikubali.

MASTAA WALIOPONZWA
Wapo mastaa wa fani mbalimbali Bongo ambao wamewahi kutajwa kuwa wanajihusisha na imani hiyo kutokana na utajiri mkubwa wa haraka na mvuto wao katika jamii.

WEMA SEPETU
Huyu ni staa wa sinema za Bongo akiwa pia Miss Tanzania kinara 2006. Yeye amekuwa akitajwa mara kwa mara kwamba, hali yake ya maisha aliyonayo siku za karibuni inatokana na kujiunga na imani hiyo.
Kwa sasa Wema, anaishi katika jumba la kifahari ambalo habari zinadai kuwa ni mali yake na aliinunua kwa shilingi milioni 400.
Mbali na jumba hilo, anamiliki magari mawili ya bei kubwa (Lexus na Verosa) ambayo si rahisi kwa Mtanzania wa mshahara wa mwezi kununua bila kujipanga kwa muda mrefu.
Mbali na jumba na magari, samani za ndani peke yake zinaweza kumsomesha mtoto kwenye shule ya kimataifa kuanzia kidato cha kwanza hadi anamaliza na fedha nyingine zikabaki za kuanzia maisha.
Amani lilizungumza na Wema Jumatatu iliyopita na kumuuliza kuhusu madai ya watu mtaani kwamba yeye amejiunga na Freemason ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Unajua mtu akiwa Freemason hawezi kujitangaza, hayo ndiyo masharti. Hao wote wanaojitangaza ujue si Freemason.”
Alipokumbushwa kuwa mbona Jayantilal Kashavji maarufu kama ‘Sir Andy Chande’ ameweka ‘pleini’ kuhusu kuwa memba wa imani hiyo, Wema alijibu:
“Yule ni kiongozi, lazima aseme vile, lakini kwa watu wa kawaida si rahisi kujitangaza.”
Alipoulizwa nini tamko lake kuhusu madai ya watu, staa huyo hakukubali wala kukataa kwamba ni mwanachama wa Freemason.

MAREHEMU STEVEN KANUMBA
Huyu hakuwahi kuweka wazi yeye mwenyewe, lakini alihusishwa kutokana na baadhi ya mavazi yake kuwa na ‘vijialama’ ambavyo ni nembo ya Freemason sanjari na mafanikio yake ya haraka kupitia filamu zake kwa Kampuni ya Kanumba The Great.
Hata hivyo, baada ya kifo chake wapo waliojitokeza kwenye vyombo vya habari wakidai walifahamu siku nyingi kuwa, msanii huyo ni Freemason.
Wengine walidiriki kusema jinsi alivyojiunga huku wakiitaja filamu yake maarufu ya Devil Kingdom kuwa ni chanzo cha kifo chake kwa sababu ndani ya muvi hiyo marehemu alitoa siri za imani hiyo.

JACQUELINE WOLPER
Naye anatembelea dalili za wenzake, siku za hivi karibuni mwanadada huyu amefanikiwa kumiliki magari matatu likiwemo moja ambalo lilimgharimu shilingi milioni 270.
Awali ilidaiwa kuwa gari hilo alinunuliwa na mchumba wake, Dallas lakini za ‘chinichini’ zikasema si kweli, ni matunda ya Freemason na ndiyo maana amefanikiwa sana.
Mbali na magari hayo, staa huyo ana miradi kadhaa ambayo ni siri ingawa zinavujavuja, lakini pia anaishi kwenye jumba la kifahari, Mbezi, Dar es Salaam ambalo hajawahi kukiri wala kukataa kwamba yeye ndiye mmiliki.
Aliwahi kuulizwa na gazeti ‘dugu’ moja na hili, Risasi Jumamosi kuhusu kudaiwa kujiunga na imani hiyo, ambapo alijibu nje ya hoja.

NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’
Ni msanii wa Bongo Fleva. Hatofautiani sana na mastaa wengine, naye anadaiwa amejiunga siku za karibuni nchini Uingereza ndiyo maana mafanikio yake yanakwenda vizuri. Msanii huyo amejenga ‘majumba’ mawili, Mbezi, Dar.
Mbali na kudaiwa kuwa aliingia Freemason kusaka utajiri, lakini pia inasemekana alifuata mvuto kwa wapenzi wake wa muziki.
Alipoulizwa alikana akidai watu wanasemasema sana. Akaulizwa kuhusu picha ambayo alipiga na mzungu mmoja wakigusanisha mikono kama alama ya Freemason, akajibu:
“Nakumbuka tukio hilo lilikuwa Uingereza, lakini mtu huyo alining’anga’nia kupiga picha hiyo bila mimi mwenyewe kutaka. Pengine pale ndiyo
Freemason, akajibu:
“Nakumbuka tukio hilo lilikuwa Uingereza, lakini mtu huyo alining’anga’nia kupiga picha hiyo bila mimi mwenyewe kutaka. Pengine pale ndiyo alinichomekea.”
JB
Anaitwa Jacob Steven ‘JB’. Ni staa wa filamu Bongo. Yeye wengi wanamhusisha kwenye imani hiyo kutokana na mvuto wake. Amekuwa akiwakosha watu kutokana na uigizaji wake, lakini wengi wanasema hapana, si uchezaji wake, anatumia kafara la Freemason kuvuta watu.

VINCENT KIGOSI ‘RAY’
Mafanikio yake makubwa yamekuwa yakienda sanjari na rafiki yake kipenzi, marehemu Steven Kanumba. Ray alipofungua kamapuni ya RJ, muda mfupi Kanumba akafungua The Great. Hata magari, kila mmoja alifanya vile mwenzake ameanza. Wengi wamekuwa wakisema walijiunga Freemason pamoja.
Ray amekuwa akikanusha kila mara kwamba, mafanikio yake ni Mungu aliyeumba mbingu na nchi na imani anayoishikilia ni ukristo.

DOKTA CHENI
Wengi wanamjua kwa jina hilo, lakini jina halisi ni Mohsin Awadh. Yeye pia ni staa wa sinema za Bongo. Kuna wakati anapotea, wakati anapanda. Lakini katika kupotea kwake, ikajagundulika kwamba ni mfanyabiashara mkubwa nchini. Anamiliki mabasi yaendayo mikaoni achilia mbali daladala za jijini Dar ambazo zimeandikwa Dokta Cheni.
Kama wenzake, alipowekwa ‘mtukati’ na kusomewa mashitaka yake kuhusu madai ya kujiunga na imani ya wenzake, alikanusha vikali akidai Watanzania si wa kuwasikiliza sana.
“Unajua kaka (paparazi) baadhi ya Wabongo si wa kuwasikiliza sana. Wanaongea mengi, hata mambo ambayo mtu hayaungi kwa njia yoyote ile,” alisema staa huyo.

JE, KWA VIONGOZI WA KISIASA?
Kundi hili ni lile lenye wanasiasa wenye mvuto mkubwa katika jamii ambapo kila njia inayofanywa ili warudi chini inashindikana, hapo ndipo Wabongo wanaposambaza maneno kuwa eti ni Freemason wakati wenyewe hawajawahi kusema wala kuonesha dalili ya kuwa katika imani hiyo.
Mfano; Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Harrison George Mwakyembe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Zubeir Kabwe, Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk. Williboard Peter Slaa.
Wengine ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Kajumulo Tibaijuka na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyayi Lowassa.
Kung’aa kisiasa kwa viongozi hawa ndiko kunakofanya baadhi ya mitandao na vinywa vya watu mitaani kuwatajataja.

LOWASSA
Huyu ni mwana CCM ambaye inadaiwa nyota yake inashindikana kuzimwa. Kila mpango unaposukwa, anavuka na kwenda hatua ya mbele yake.
Juzikati, kuna baadhi ya viongozi wa kidini walidiriki kutabiri kuwa, kasi yake ya kwenda ikulu haiepukiki kutokana na nyota yake kung’ara kupita kiasi.

KALAMU YA MHARIRI
Kama kichwa cha habari kinavyosema; NANI FREEMASON, NANI SIYE? Imefika hatua sasa Watanzania waache mara moja kuwataja watu kuhusika na kitu fulani kwa mitazamo yao bila wenyewe kuweka wazi.
Itafika mahali taifa litakumbwa na mvurugano ambao hauna maana na mbaya zaidi wasababishaji watakuwa wetu wengine kabisa mbali na wahusika.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------

MSANII WA CHUZ NUSURA AACHIKE KWA MUMEWE

Na Erick Evarist
HAUSIGELI kwenye Tamthiliya maarufu ya Milosis, Erica Swilla ‘Kijakazi’ anadaiwa kunusurika kuachwa na mumewe, Daniel ambaye ni askari wa jeshi la polisi kufuatia msanii huyo kuanza tabia za kuchelewa kurejea nyumbani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘Elly’ ambaye amecheza tamthiliya hiyo katika nafasi ya mfanyakazi wa ndani ‘hausigeli’ aliruhusiwa na mumewe kushiriki sanaa kwa masharti ya kuwahi kurejea nyumbani.
“Alipewa masharti ya kurudi nyumbani mapema lakini baada ya kuanza kuonekana runingani, amebadilika tabia na kuanza kuchelewa nyumbani,” kilisema chanzo.
Erica mwenyewe alipopatikana na kusomewa mashitaka yake, alisema ishu si kuchelewa bali ni kuwekana sawa kama wanandoa.
“Ishu si kuchelewa, ila sisi kama wanandoa lazima kukumbushana, ni wajibu wake kunisisitizia majukumu,” alisema Erica.
    Chanzo cha habari ni kutoka Gazeti la Amani

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate