WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapenzi wa
klabu kongwe za Simba na Yanga wanatarajiwa kuumana katika soka wakati
wa Tamasha la Matumaini litakalorindima Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam Julai 7, mwaka huu.
Tamasha hilo linatarajiwa kushirikisha mechi mbalimbali za soka na
ndondi, ambapo mbali na mechi ya wabunge, Bongo Movie na Bongo Fleva
wataumana huku Jitegemee wakioneshana kazi na Makongo, huku kwenye
masumbwi Japhet Kaseba atazichapa na Francis Cheka, ambapo watatanguliwa
na mapambano mengine kadhaa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa matukio wa Dar Live,
Abdallah Mrisho, ambao ndiye waandaaji wa tamasha hilo, alisema lengo
kubwa la tamasha hilo ni kuhimiza umuhimu wa kuendelea kuishi kwa
pamoja, kuliombea taifa na kuchangia mfuko wa elimu.
Aidha, Mrisho alisema, katika tamasha hilo asilimia 20 ya mapato
yatakwenda mfuko wa elimu kwa ajili ya kusaidia kununulia madawati na
mambo mengine mbalimbali, ambapo wameamua hivyo baada ya kuombwa na
wahusika.Aliongeza kuwa, tamasha hilo litapambwa na wasanii Naseeb Abdul
‘Diamond’ Joseph Muyanja ‘Chameleon’ kutoka Uganda na wengineo.
Habari na Clescencia Tryphone wa Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment