Juzi ilikuwa siku ya watoto duniani. Lakini wakati watoto
wakisherehekea na kukumbuka haki zao za msingi, hali kwa mtoto Abdillahi
Juma (10), ambaye amekuwa akiugua maradhi ya polio kwa muda mrefu
imekuwa ni tofauti, baada ya wazazi wake kudaiwa kumfungia ndani bila
matibabu kwa miaka minane.Kugundulika kwa mateso hayo kulitokana na
kuzagaa kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Iyoli,
Kata ya Kingali, kilomita 30 kutoka Kondoa Mjini kuhusu mtoto huyo
ambaye alipooza tangu akiwa na umri miaka miwili.
Baada ya kupata taarifa hiyo, mwandishi wa habari hii alifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo kupata ukweli wa suala hilo.Alimkuta mtoto huyo akiwa katika hali mbaya hivyo kutumia muda mwingi kuwashauri wazazi wake wampeleke hospitali. Hata hivyo, badala ya kubeba jukumu hilo, walimruhusu mwandishi kumpeleka hospitali. Baada ya kupata ruhusa hiyo alimpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa na baadaye Ofisi ya Ustawi wa Jamii ya Wilaya ambako alipokewa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa, John Ruwanda alisema alichunguzwa na kusema anaendelea vizuri.
Hata hivyo, Dk Ruwanda alishauri mtoto huyo aendelee na matibabu na kuwa katika uangalizi maalumu... “Ni hatari kwa binadamu kufungiwa ndani kwa kipindi kirefu akiwa peke yake tena mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli.”
Ili kumuondolea madhila hayo, Ruwanda alisema: “Ni vyema kwa sasa awepo katika kituo cha huduma ili tuangalie namna ya kumsaidia na kupata msaada zaidi.”

Dk Ruwanda alisema wananchi wengi wamekuwa na
utaratibu wa kujiamulia masuala muhimu ya kijamii wenyewe bila kutaka
ushauri kutoka kwa watu wengine dhamana ya kutatua matatizo
yanayowakumba.
Alisema hali hiyo imekuwa ikiwaathiri kiafya na wakati mwingine kukumbuka umuhimu wa kuwapeleka hospitali wakiwa mahututi.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Hamis Isaka alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema: “Nilishawahi kuwashauri waende katika kituo cha afya. Niliwahi pia kuwaeleza wamsaidie kwa kumpatia mtu wa kushinda naye wakati wanaendelea na shughuli nyingine za kazi mchana lakini sijui wenzangu walifikiria nini.”
Baba wa mtoto
Baba wa mtoto, Juma Issa alisema walihangaika naye kwa muda mrefu tangu alipoanza kupata homa akiwa na miaka miwili lakini, kutokana na matatizo ya kukosa fedha walishindwa kuendelea na huduma za matibabu.
“Baada ya kupata homa tulihangaika kumpeleka katika zahanati na baadaye kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ambako alipatiwa tena tiba na kuruhusiwa, isipokuwa muda ulivyozidi kwenda ndivyo homa ilivyozidi kumuumiza na sisi tukawa tumeishiwa fedha.”
“Tulikata tamaa baada ya kuona anazidi kubadilika viungo na kuwa mlemavu na sisi hatuna utaalamu wowote wa kujua kama anaweza kupona au vipi. Pia hatuna elimu juu jambo kama hili ndipo tulichoka na kukata tamaa kabisa.
Kuhusu kumfungia ndani peke yake hasa nyakati za mchana, alisema inatokana na wao kukosa mtu wa kumwacha naye wanapokuwa wamebanwa na kazi hasa za kilimo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Steven alisema hana taarifa kuhusu suala hilo lakini akasema: “Nashukuru kujulishwa nitafuatilia na kuifanyia kazi taarifa hii.”
Chanzo cha habari ni Gazeti la Mwananchi na Shakila Nyerere, Kondoa.

No comments:
Post a Comment